WATOA HUDUMA WA MATUKIO

Huduma yako, mbele ya kila tukio.

Ukumbi, MC, mapambo, chakula, mziki, picha au usafiri — jiunge na AsanteSana, onyesha kazi zako, pokea maombi ya booking kutoka kwa wanaoandaa matukio, na ulipwe kwenye simu.

  • Kujiunga ni bure
  • Unalipa tu ukipata kazi
  • Mteja analipa 40% kushikilia tarehe

INAVYOFANYA KAZI

Dakika mbili, hatua tatu

01
Jisajili bure

Jina la biashara, aina ya huduma, mji na namba ya simu.

02
Jaza profile yako

Picha za kazi zako, bei zako na siku zilizo wazi kwenye kalenda.

03
Pokea kazi, ulipwe

Maombi yanafika kwenye dashboard yako. Unakubali, unafanya kazi, unatoa pesa kwenye simu.

UNACHOPATA

Kila kitu cha kupata na kusimamia kazi

Profile ya kushiriki

Ukurasa wako wenye kazi zako, link na QR — mtumie mteja kwenye WhatsApp, iweke dukani.

Kalenda na maombi

Siku zilizo wazi zinaonekana, maombi yanafika mahali pamoja — hakuna booking mbili siku moja.

Malipo salama

Mteja analipa 40% kushikilia tarehe. Pesa yako inaingia kwenye salio lako, unaitoa kwenye simu.

Wateja kutoka matukio

Wanaoandaa harusi, send-off na makongamano kwenye AsanteSana wanakuona na kukuweka kwenye matukio yao.

GHARAMA, WAZI

10% tu, na ukipata kazi pekee

Hakuna ada ya kujiunga wala ya mwezi. Kwenye kila booking, 5% inatoka kwenye bei yako na 5% inaongezwa kwa mteja — hakuna upande unaobeba yote. Mfano: ukitaja TZS 1,000,000, mteja analipa TZS 1,050,000, na wewe unapokea TZS 950,000.

Unapokea kwa kazi ya TZS 1,000,000TZS 950,000

AINA ZA HUDUMA

Kila anayehitajika kwenye siku kubwa

KumbiUkumbi wa harusi, sendoff, mikutano na makongamano.
MCMwendesha shughuli anayeshika siku yako.
WapambajiMapambo ya ukumbi, maua, taa na jukwaa.
Chakula na vinywajiUpishi, huduma ya mezani na vinywaji.
MzikiBendi, DJ, kwaya na vifaa vya sauti.
UsafirishajiMagari ya harusi, mabasi ya wageni na mizigo.
Maids na best menTimu ya maharusi na mavazi yao.
Picha na videoWapiga picha, video na drone.
KekiKeki za harusi, sendoff na sherehe.
MavaziGauni, suti, vitenge na ushonaji.
UremboMake-up, nywele na kucha.

Wateja wako wa msimu ujao wanaandaa matukio sasa hivi.

Jisajili bure

Una akaunti tayari? Ingia · Organizer alishakuweka kwenye tukio lake? Dai profile yako